KISANGARA TOURS, YAIPONGEZA SERIKALI KWA KUIMARISHA SEKTA YA UTALII


MWANGA-KILIMANJARO.

KAMPUNI ya utalii ya Kisangara Tours Limited imeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa inazozifanya katika kukuza na kuimarisha sekta ya utalii nchini, ikisema jitihada hizo zimeleta mafanikio makubwa katika kuitangaza Tanzania kimataifa.

Kauli hiyo ilitolewa Disemba 27,2025 na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Frida Mberesero, wakati wa Tamasha la Mwanga Utalii Festival and Marathon, lililofanyika katika uiwanja wa C.D. Msuya,

Mberesero alisema; kampuni hiyo inatambua mchango wa serikali katika kuboresha mazingira ya biashara ya utalii, hususan kupitia kampeni ya Tanzania Royal Tour, ambayo imeongeza hamasa ya watalii wa ndani na nje ya nchi.

Alisema kampuni yake itaendelea kushirikiana na serikali kwa vitendo kwa kuwa balozi mzuri wa utalii, kwa kuitangaza Tanzania kama kitovu salama na chenye vivutio vya kipekee vya utalii.

“Kama wadau wa utalii, tuna kila sababu ya kuishukuru serikali kwa jitihada zake, Kampeni ya Tanzania Royal Tour imetupa mwelekeo na sisi tumejipanga kuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza nchi yetu,” alisema Mberesero.

Alifafanua kuwa Kisangara Tours Limited, yenye makao makuu yake jijini Arusha, inajihusisha na uandaaji, upangaji na uendeshaji wa safari za utalii ndani na nje ya nchi, kwa lengo la kutoa huduma bora zinazozingatia ubora, usalama na uendelevu wa mazingira.

Aidha aliongeza kuwa kampuni hiyo imejikita katika kutangaza na kukuza utalii na michezo Wilayani Mwanga, kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira, ubunifu na matumizi ya uzoefu wa kitaalamu ili kuifanya Mwanga kuwa miongoni mwa maeneo muhimu ya utalii nchini.

"Tangu kuanzishwa kwa tamasha hili mwaka 2024, yako mafanikio makubwa ambayo yameonekana ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya watalii kutembelea vivutio, fursa za ajira kwa vijana wanaowatembeza watalii, sanjari na kukuza utamaduni na sanaa za asili kupitia maoneshi na burudani,"alisema.

Alisisitiza kuwa ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi na jamii ni nguzo muhimu katika kukuza utalii endelevu na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika maendeleo ya taifa.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.