MWANGA-KILIMANJARO.
ONGEZEKO la idadi ya watalii wanaotembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini limeendelea kuongeza pato la taifa na kuingiza fedha za kigeni, hatua inayochangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, wakati akizungumza katika hafla ya kuhitimisha Tamasha la Mwanga Utalii Festival and Marathon, lililofanyika katika Uwanja wa C.D. Msuya wilayani Mwanga.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan aalifanya kazi kubwa ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, jambo lililopelekea kuongezeka kwa idadi ya watalii wanaotembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Mlima Kilimanjaro na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.
Aidha, Mkuu wa Mkoa alimpongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Kisangara Tours kwa kuanzisha tamasha hilo ambalo limefanikiwa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya Wilaya ya Mwanga ambavyo vingi havikuwa vikijulikana hapo awali.
Katika hatua nyingine, Babu alitoaa maelekezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa kuhakikisha kikosi cha jogging cha mkoa kinashiriki katika tamasha hilo mwakani, akisisitiza kuwa sekta ya utalii ina mchango mkubwa katika kuwainua vijana, wanawake na wajasiriamali wadogo kiuchumi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Rukia Ally Zuberi, amesema wilaya hiyo imeendelea kutekeleza maelekezo ya Rais Samia kwa kushirikiana na wadau wa utalii, akitaja Kampuni ya Kisangara Tours kuwa mshirika muhimu katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo wilayani humo.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mwanga, Ibrahim Mnzava, amesema kuanzisha tamasha hilo, limekuwa kiunganishi muhimu cha wakazi wa Mwanga wanaoishi ndani na nje ya wilaya hiyo.
Akisomwa risalaa ya Tamasha hilo Mwenyekiti wa Mwanga Utalii Festival and Marathon Frida Mberesero, amesema tamasha hilo limekuwa chachu ya kukuza utalii wa ndani, kuibua fursa za ajira, kukuza sanaa na utamaduni








