UWT MOSHI MJINI, WATETEZI WA MAMA SAMIA WAFANYA MATEMBEZI YA KUOMBA KURA KWA WANANCHI

MOSHI-KILIMANJARO.

Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Moshi Mjini kwa kushirikiana na Taasisi ya Watetezi wa Mama Samia, wamefanya matembezi maalum ya kuwaombea kura wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuelekea uchaguzi wa Oktoba 29, mwaka huu.

Akizungumza Oktaba 25,2025, wakati wa matembezi hayo, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Moshi Mjini, Theresia Komba, alisema lengo la shughuli hiyo ni kutoa hamasa na kuonyesha sapoti kwa wagombea wa CCM kwa kuwatembelea wafanyabiashara, machinga na wajasiriamali mbalimbali, ili kuwaomba wawapigie kura siku ya uchaguzi.

Komba aliongeza kuwa kupitia kampeni hiyo, wameendelea pia kuhamasisha wananchi wote kujitokeza kwa wingi kushiriki kupiga kura, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni haki ya kikatiba kwa kila Mtanzania.

Kwa upande wake, Dk. Niever Zekeya, aliyewahi kuwa mtia nia wa ubunge wa viti maalum Mkoa wa Kilimanjaro, alisema matembezi hayo yamefanyika katika maeneo mbalimbali ikiwemo Stendi Kuu ya Mabasi ya Moshi, Posta, na maeneo ya biashara.

Alisema lengo kuu ni kuwaombea kura wagombea wa CCM, akiwemo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Ibrahim Shayo, pamoja na Diwani wa Kata ya Mawenzi, Apaikunda Naburi.








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.