NJORO-MOSHI.
Mgombea udiwani wa Kata ya Njoro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhandisi Zuberi Kidumo, ameahidi kuhakikisha kata hiyo inakuwa kinara wa kutoa kura nyingi kwa CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni, Kidumo amesema wananchi wa Njoro wanapaswa kuchagua viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya juu hadi chini ili kuendeleza miradi ya maendeleo na kuongeza ustawi wa wananchi.
“Tujitokezeni Oktoba 29, mwaka huu tulamchague mgombea urais wa CCM Dk. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wetu Ibrahim Shayo, na mimi Zuberi Kidumo kuwa Diwani wenu, tukifanya hivyo, tutajihakikishia kasi ya maendeleo na miradi mikubwa inayoendelea katika kata yetu,” alisema Mhandisi Kidumo.
Alieleza kuwa CCM imeonyesha dira ya kweli ya maendeleo kwa wananchi, na kwamba kwa ushirikiano wa karibu kati ya Serikali Kuu, Bunge na Halmashauri ya Kata, Njoro inaweza kuwa mfano wa mafanikio kwa kata nyingine zioizopo katika Manispaa ya Moshi,"alisema.
Mgombea huyo wa udiwani kata ya Njoro alihitimisha kwa kuwataka wananchi wajitokeze kwa wingi siku ya uchaguzi, wakijua kuwa kura zao ni chombo cha kuleta mabadiliko chanya katika maisha yao ya kila siku.















