Kauli Mbiu: "Bondeni Yetu, Fahari Yetu Sote"
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Bondeni – Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, walifanya uchaguzi wa kura za maoni tarehe 4 Agosti 2025 kwa ajili ya kupata wagombea wa nafasi ya udiwani kwa uchaguzi mkuu wa Tanzania Bara.
Katika uchaguzi huo, jumla ya wagombea wane walichuana kuwania nafasi hiyo, ambapo Hajji Fundi Hajji aliibuka kidedea kwa kupata kura 106, akiwapiku wagombea wenzake kwa tofauti kubwa. Nafasi ya pili ilichukuliwa na John Hamaro aliyepata kura 28, akifuatiwa na Masiu Amiri Kilusu aliyepata kura 22, huku Omary Salim Ninga akiambulia kura 4 pekee.
Ushindi huo wa Hajji Fundi Hajji umeonesha kuungwa mkono kwa nguvu na wajumbe wa chama katika kata hiyo, ishara ya imani waliyonayo juu ya uwezo wake wa kuiongoza Bondeni na kusimamia vyema Ilani ya CCM kwa kipindi kijacho.

