VILABU 40 KUSHIRIKI MASHINDANO YA ZUBERI CUP TOURMENT MSIMU WA TANO


MOSHI-KILIMANJARO

Mshinndano ya Zuberi Cup Tourment-2025  msimu wa tano yanatarajiwa kuanza kurindima Julai 20 mwaka huu, katika uwanja wa Railway uliopo Kata  ya Njoro Manispaa ya Moshi, huku vilabu 40 vikitarajiwa kushiriki mashindano hayo.

Akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzinwa mashindano hayo iliyofanyika katika uwanja wa wazi wa Hugo's uliopo mjini hapa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo, ameahidi kuendelea kushirikiana na mwaandaji wa mashindano hayo kadri Mungu atakavyomwezesha.

Katika hotuba yake Tarimo, amekishukuru Chama cha mpira wa mgigu mkoa, Wilaya na Wadau wa mchezo kwa kujitoa kwao na kutoa rasilimali zao katika kusapoti mchezo huo.

Pia mbunge Tarimo amempongeza Mhandisi Zuberi Abdallah Kidumo kwa kazi nzuri ya kujitoa kwake na kufanikisha kujenga wa uwanja wa kisasa wa mpira, jambo ambalo limewezesha kupanua wigo wa timu nyingi  kushiriki katika ligi.

Amesema  katika mashindano ya msimu huu wa tano ameahidi  kutoa zawadi ya sh Ml 10, ambapo mshindi wa kwanza atapata Sh ml 4, mshindi wa pili ml 3, mshindi wa tatu ml 2 na mshindi wa 4 kuondoka na Sh ml 1.

Aidha amesema Manispaa ya Moshi inakabiliwa na changamoto ya viwanja vya kuchezea mpira wa miguu, huku akiahidi kwamba ataenda kuushawishi uongozi wa Manispaa hiyo, ili uwanja wa Majengo Stadium uweze kutumika katika mashindano ya zuberi Cup Tourment-20

Akizungumza mwaandaaji wa mashindano hayo ma Meya mstaafu wa Manispaa ya Moshi Mhandisi Zuberi Abdallah Kidumo, amemshukuru Mbunge Tarimo kwa kuendelea kudhamini mashindano hayo ambayo kwa sasa yamekuwa na ushiriki mkubwa 

"Huu ni msimu wa tano tangu kuanzisha mashindano haya, na mwanzo kabisa ilikuwa ni kwa ajili ya ligi kata ya Njoro, lakini baada ya kuona watu wanapenda mpira mashindano haya niliweza kutoa uwanda mpana ili kila kata zilizoko katika Manispaa ya Moshi ziweze kushiriki jambo ambalo kumekuwa na ari kubwa,"amesema.

Amesema wakati tunaaza mashindano hayo walianza katika mazingira magumu kutokana na uwanja kuwa Railway kuwa sio rafiki lakini vijana walicheza na kuweza kufanikiwa vizuri.

Naye Mwenyekiti wa mashindano ya Zuberi Cup Tourment 2025 Mwl. Japhet Mpande, amesema zaidi ya timu 40 zitashiriki katika mashindano hayo , huku akitoa wito kwa wakazi wa Manispaa ya Moshi kushiriki katika mashindao hayo .





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.