MADIWANI WA VITI MAALUM 17 WAANGUKIA PUA KILIMANJARO, BAADA YA KUBWAGWA NA WAJUMBE WA UWT

KILIMANJARO.

Madiwani wa viti maalum 17 waliokuwa wakitetea nafasi zao katika Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Kilimanjaro, wameangukia pua baada ya kubwagwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum ulioketi kwa ajili ya  mchujo wa kura za maoni ndani ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT).

Mchujo wa kura za maoni kwa nafasi ya madiwani wa viti maalumu ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)ulikamilika Julai 20, mwaka huu, ambapo madiwani 17 kutoka halmashauri za mkoa huo wakigalagazwa na watia nia wapya walijitokeza kuomba nafasi hiyo   kwa ajili ya kwenda kuwawakilisha katika halmashauri za mkoa huo.

Mchujo huo uliofanyika Julai 20,2025, ambapo ulihusisha upigaji kura ya maoni kwa ajili ya kuwapata wagombea wa nafasi za viti maalum ya udiwani kwa uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Baadhi ya majina makubwa na waliokuwa maarufu katika siasa za maeneo yao wameondolewa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Kwa Wilaya ya Moshi Vijijini madiwani waliobwagwa ni pamoja na: Aurelia Mushi, Anna Lyimo, Mwajabu Mchomvu, Fabiola Massawe, Theresia Mlay, Christina Mchau, Adelina Temba. Wilaya ya Rombo: Anna Silayo Pius, Getridi Kimario. Wilaya ya Hai: Amina Sway, Halima Mdee, Eusen Nkya.

Wilaya ya Mwanga: Anzilani Mfinanga, Wilaya ya Moshi Mjini: Stella Kasese Wilaya ya Siha, Sauda Leman a kwa Wilaya ya Same waliobwagwa ni: Veronica Mzava na Habiba Iringo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.