MAHENDEKA AWATAKA WATUMISHI WA TAKUKURU KUFANYA KAZI KWA UADILIFU NA UZALENDO


                                         ROMBO-KILIMANJARO 

Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kote nchini wametakiwa kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi, uadilifu na uzalendo, huku wakifuata Sheria, Kanuni na Taratibu zote katika kuwahudumia wananchi.

Kauli hiyo  ilitolewa Juni 19,2025  na mwakilishi wa Katibu Mkuu Ikulu, Neema Jamu, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro.

“Mtumishi bora hana muda wa kulalamika, bali hutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili watu anaowahudumia,” alisema Mahendeka.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Ikulu lisema jengo hilo lenye ukubwa wa mita za mraba 240 limejengwa kwa gharama ya Shilingi milioni 290, na linalenga kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa TAKUKURU katika wilaya hiyo pamoja na kuimarisha huduma kwa wananchi.

Katika tukio hilo, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Neema Mwakalyelye, alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake imara na kwa kuendelea kuiwezesha taasisi hiyo kwa rasilimali watu, fedha na vitendea kazi.

Mwakalyelye alibainisha kuwa chini ya Serikali ya Awamu ya Sita, TAKUKURU imeweza kutekeleza ujenzi wa majengo mapya ya ofisi katika mikoa na wilaya mbalimbali nchini kupitia mfumo wa Force Account kwa kuzingatia Sheria ya Manunuzi ya Umma Na. 7 ya mwaka 2011 (Sura ya 410) na kanuni zake za mwaka 2013, kama zilivyorekebishwa mwaka 2026.

Alisema mwaka wa fedha 2021/2022, Takukuru ilijenga majengo sita : Majengo 6 (Kilimanjaro, Mvomero, Kongwa, Kilolo, Kiteto, Liwale)  

Alisema kuwa mwaka 2021/2022 Takukuru imejenga majengo sita likiwemo jengo la mkoa Kilimanjaro,  jengo la wilaya ya Mvomero,  Kongwa, Kilolo, Kiteto na Liwale.

Aidha alisema mwaka 2022/2023 walijenga majengo matano mkoa wa Simiyu, Iringa, wilaya ya Momba,  Nyasa pamoja na jengo maalumu la kazi za uchunguzi Safe House, huku majengo sita yakijengwa mkoa wa Shinyanga, Wilaya ya Monduli, Kishapu, Nkasi, Nzega na Wilaya ya Rombo.

Alifafanua kuwa mwaka 2024/2025 Takukuru inaendelea na ujenzi wa majengo nane  katika mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Kiliua, Rungwe, Mbulu, Ukerewe, Makete, Nyang’wale na Mafia

Alisema, "Kwa takwimu hizi, Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwa TAKUKURU, jambo linalodhihirisha dhamira ya dhati ya Rais Samia katika mapambano dhidi ya rushwa nchini."

Kwa upande wake, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kilimanjaro, Musa Chaulo, alielezea historia ya ofisi hiyo, akibainisha kuwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002, TAKUKURU Rombo ilikuwa ikifanya kazi kwenye jengo la kupangisha la KNCU, hali iliyokuwa inakwamisha ufanisi wa kazi na uhuru wa wananchi kufika kutoa taarifa au malalamiko.

"Kupitia jengo hili jipya, ari ya watumishi imeongezeka, na wananchi sasa wanatufikia kwa uhuru zaidi, wakipata huduma kwa karibu na kwa wakati," alisema Chaulo.

Aidha, aliongeza kuwa jengo hilo limewawezesha watumishi kufanya kazi katika mazingira rafiki na salama, na kwamba huduma za uchunguzi, uzuiaji wa rushwa, uelimishaji wa umma na mashtaka sasa zinapatikana kwa ufanisi mkubwa zaidi ndani ya Wilaya ya Rombo.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.