RAIS DKT. SAMIA AWASILI KILIMANJARO KUSHIRIKI MAZISHI YA HAYATI MZEE CLEOPA MSUYA

KILIMANJARO, 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)leo jioni kwa ajili ya kushiriki mazishi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Mzee Cleopa David Msuya.

Mara baada ya kuwasili, Rais alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, ambapo alipata fursa ya kusalimiana nao kabla ya kuelekea Wilayani Mwanga, ambako mazishi ya Mzee Msuya yanatarajiwa kufanyika Mei 13 2025, kijijini kwake Usangi alikozaliwa.

Hayati Msuya, alifariki dunia Jumatano ya Mei 7,2025  Kijitonyama Jijini Dar es Salaam  alipikuwa akipatiwa matibabu ya moyo, na kwamba Taifa limeendelea kuomboleza kifo chake kwa majonzi makubwa.

Mazishi hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa kitaifa, viongozi waandamizi wastaafu, wananchi, pamoja na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.