Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mwl. Mwajuma Nasombe,
amesema kuwa kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya
sita Manispaa hiyo imekuwa kimapato kutoka asilimia 32 hadi kufikia asilimia
75.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake jana Mwl. Nasombe
amesema kuwa kuongezeka kwa mapato hayo kumechangiwa na miundombinu sahihi ya
ukusanyaji wa mapato,
Mwl. Nasombe amesema kuwa katika upande wa ushuru wa masoko makadirio
kwa mwaka ni kukusdanya kiasi cha Sh milioni 298 ambapo mpaka sasa tayari wamekusanya
Sh milioni 220 jambo ambalo linaonesha kuwa huwenda wakavuka makadirio hayo.
Aidha amesema kuwa Manispaa hiyo iliamua kukusanya mapato yenyewe baada
ya kuona kuwa mawakala walikuwa wameshuka kiwango kilichokuwa kimekusudiwa.
