MOSHI.
Mamlaka ya Mapato Tanzania
TRA Mkoa wa Kilimanjaro wametoa msaada wa mahitaji muhimu kwa wafungwa na mahabusu
wanaotumikia kifungo katika Gereza la Karanga ikiwa sehemu ya kurejesha kwa
jamii katika kuelekea siku ya wiki ya Shukrani kwa Mlipa kodi.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi msaada huo Meneja wa TRA Mkoani hapa James Jilala wamesema wameona ni
vema kuwashika mkono wafungwa hao ambao wana uhitaji mkubwa.
“Tunafahamu kwamba serikali
inafanya jitihada kubwa katika kuwahudumia wafungwa na mahabusu walioko
magerezani, lakini na sisi TRA tumeona tuje kuwashika mkono wenzetu hawa
walioko hapa gerezani ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa mlipa kodi.”alisema.
“Mamlaka ya mapato Tanzania, tuliona ni muhimu kujumuika na wenzetu hawa, ambapo leo tumekuja kuwakabidhi magodoro 50 gereza kuu la Karanga,”alisema Jilala.
Akipokea msaada wa magodoro
50 yaliyotolewa na TRA mkoani hapa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna
Msaidizi wa Magereza SACP Leornad Burushi,alisema mahitaji ni makubwa na kwamba
bajeti ya serikali haitosherezi mahitaji ya gereza hilo lenye wafungwa wengi.
“Magodoro ambayo yamekuwa
yakinunuliwa na serikali hayatosherezi mahitaji ya wafungwa na mahabusu walioko
katika gereza hilo, tunawashukuru sana TRA kwa kutuletea magodoro haya hapa
gereza kuu Karanga,”alisema.
Alisema kuwa TRA sio mara yao ya kwanza kuleta misaada hapa, wamekuwa wakitukumbuka katika nyakati tofauti na kwa msaada huu kwetu unakwenda kupunguza changamoto iliyop,” alisema.
