Diwani Arusha Chini aishukuru Halmashauri ya Moshi Vijijini kwa kutoa Sh bilioni 1.26 matengenezo ya barabara


MOSHI.

Diwani wa Kata ya Arusha Chini Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, mkoa wa Kilimanjaro Leonard Waziri, amelishukuru Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo kwa kuitengea kata hiyo kiasi cha Sh bilioni 1. 26 kwa ajili ya matengenezo ya barabara zilizoko ukanda wa Arusha Chini.

Hayo aliyasema jana wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha miata mitano kuanzia mwaka 2020 hadi Februari 2025, ambapo amesema endapo serikali itakamilisha ukarabati wa barabara katika kata hiyo italeta matokeo chanya kwa wananchi na kuendelea kukiamini chama hicho.

Alisema ubovu wa miundombinu ya barabara katika Ukanda wa Arusha Chini kimekuwa kilio cha muda mrefu kwa wananchi wa kata hiyo hali ambayo imekuwa ikiwapa changamoto kubwa ya usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali  kwenda masokoni hususan katika kipindi cha mvua.

“Katika kitu kinachonitesa kwenye kata yangu ni changamoto ya barabara, kilio hiki kimekuwa cha muda mrefu sana, nalishukuru baraza la madiwani kwa kukubali ombi langu la kunitengea Sh bilioni 1.26 kwa ajili ya ukarabati wa barabara kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato,”alisema Diwani Waziri.

Alizitaja barabara ambazo zimekuwa changamoto kupitia katika kipindi cha mvua ni pamoja na barabara ya Mawala-Mikocheni, barabara ya Samanga-Chemchem na barabara ya TPC-Samanga-Mikocheni.

Kuhusu sekta ya elimu alisema kwa kipindi hicho kata hiyo wamefanikiwa kujenga madarasa matano, mabweni mawili, na Matundu ya vyoo nane kwenye shule ya sekondari Langasan kwa Sh milioni 401.8, uwekaji wa umeme nyumba tatu za walimu  shule Msingi Chemchem.

Alisema pia wamefanikiwa kujenga shule ya sekondari ya Kata Mikocheni na hivyo kuwapunguzia adha ya wanafunzi kutembea umbali wa kilometa 34 kwenda kilometa 17 na kurudi kilometa 17.

Vile vile alisema walifanikiwa kujenga  madarasa saba shule ya Msingi Ronga, sambamba na kuweka mpango bora wa matumizi ya ardhi, ujenzi wa ghala la chakula Chemchem, ujenzi wa ofisi ya kijiji, ujenzi wa nyumba ya Uvuvi pamoja na ujenzi wa soko.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Morris Makoi ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema serikali imetenga fedha Sh bilioni 15 kwa ajili ya kuchimba mitaro mikubwa ambayo itakwenda kuzuia maji ya mvua mabayo hutoka milimani na kuishia ukanda wa chini na hivyo kusababisha mafuriko.

“Mvua za masika ambazo zimekuwa zikinyesha ukanda wa milimani, ukanda wa chini umekua ukiathiriwa sana na maji haya ambapo hutokea mafuriko na maeneo ambayo yamekuwa yakiathirika zaidi ni Kata ya Kahe Mashariki, Mabogini, Kahe Magharibi na Arusha Chini.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.