Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond, akizungumza kwenye kongamano la Wanawake na Wanaume wa Uchumi wa Viwanda Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro (WAWAUVITA) lililofanyika Kimanganuni, Kata ya Uru Kusini , Halmashauri ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro kuhudhuuriwa na Wajasiriamali takribani 250.
MOSHI-KILIMANJARO
Imeelezwa kuwa utunzaji
bora wa kumbukumbu husaidia wajasiriamali kufuatilia maendeleo ya biashara zao,
kutathmini faida na hasara na kutoa mwelekeo sahihi katika kupanga mikakati ya
ukuaji wa biashara zao.
Mwenyekiti wa Taasisi ya
Wanawake na Wanaume wa Uchumi wa Viwanda Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro
(WAWAUVITA), Mariam Muhandeni, aliyasema hayo jana wakati akizungumza katika kongamano
la (WAWAUVITA) lililofanyika Kimanganuni, Kata ya Uru Kusini na halmashauri ya
Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro kuhudhuuriwa na wajasiriamali takribani 250.
Amesema utunzaji mzuri wa
kumbukumbu za biashara , husaidia kujua muda unaopaswa kuagiza bidhaa husika
huku akisema kuwa ni makosa katika biashara kuishiwa bidhaa inayohitajiwa na
wateja kwani mjasiriamali anaweza kupoteza wateja wake.
Aidha amesema kuwa sio
vizuri kuwa na akiba ya bidhaa nyingi
ambayo hainunuliki, huku akisistiza pia ni muhimu mjasiriamali kujua hali ya kifedha ya biashara
yake, wakati wowote ili kuepuka changamoto zinazoweza kutokea.
Naye Katibu wa Wawauvita Joseph France Aloyce, amesema wajasiriamali wengi wanashindwa kufanikiwa na kupiga hatua kutokana na kukosa umakini katika kutunza kumbukumbu za biashara.
“Kadri biashara yako
inavyokua na idadi ya shughuli za kibiashara zinavyoongezeka, inakuwa vigumu
kufuatilia manunuzi, mauzo, mali, fedha taslimu, wadai na wadaiwa, hivyo kuna
umuhimu wa kuwa na kumbukumbu za biashara,”amesema Aloyce.
Akifundisha katika semina
hiyo Meneja wa Benki ya Azania tawi la Moshi Yusuf Lenga, amewataka wakazi hao
wa Uru Kusini kuachana na utaratibu wa kujiunga katika vikundi kwa nia ya
kutaka fedha.
Wengine waliopata fursa ya
kufundisha ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Beatrice
Kimaro ambaye amewataka wajasiriamali hao kujitahidi kuwa na matumizi mazuri
Awali akizungumza katika
kongamano hilo Diwani wa Kata ya Uru Kusini halmashauri ya Wilaya ya Moshi
Vijijini mkoani Kilimanjaro, Wilhard Kitali, amewataka wakulima wa ndizi kuungana
kwa pamoja katika utaratibu unaofaa ili kuhakikisha soko la zao hilo
halichezewi na wachache wanaotaka kujinufaisha kupitia wakulima hayo.
“Hali iliyopo kwa sasa kwa wakulima wa ndizi wa Uru Kusini Mkungu mmoja wa ndizi umekuwa ukinunuliwa shambani kwa shilingi 3,000 hadi shilingi 5,000, kisha unauzwa kwa zaidi ya shilingi 15,000 kwenye masoko makubwa nchini baada ya walanguzi kuchukua shambani hatua ambayo imekuwa mwiba kwa wakulima.”amesema.
Mweka Hazina wa taasisi hiyo Magreth John amesema wajasiriamali wengi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo zile za ufungashaji, upatinaji wa namba ya ubora na utunzaji fedha, kupitia kongamano hilo wazalishaji waliweza kupata fursa kukutana na wataalam mbalimbali wakiwemo wa TBS na kuweza kupata utaratibu wa namna ya kupata uthibitisho wa bidhaa zao.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond, alipata fursa ya kuzungumza na wajasiriamali hao wa Uru Kusini na kuongeza kuwa wakulima wenye elimu ya fedha wanaweza kuelewa na kuchagua mikopo bora kutoka kwa taasisi za kifedha kama vile benki na vikundi vya kifedha na kwamba kupitia mikopo hiyo, inaweza kutumika kupanua shughuli za kilimo.
“Wakati watu wanapokuwa na elimu ya fedha, wanakuwa na tabia
bora za kifedha kama vile kuwekeza, kulipa kodi, na kuchangia katika uchumi wa
taifa, hii inaongeza ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.













