Serikali Wilayani Mwanga, yaipongeza Kampuni ya Kisangara Tours Ltd

MWANGA-KILIMANJARO

Serikali Wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro  imeipongeza Kampuni ya Kisangara Tours Ltd, kwa kutoa mchango mkubwa katika kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyomo wilayani humo.

Pongezi hizo zimetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya hiyo Mwanahamisi Munkunda, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Tamasha la Mwanga Marathon and Festival-2024 ambalo limelenga kuvitangaza vivutio vya utalii, kukuza uchumi wa wananchi wa wilaya hiyo na kuhamasisha ushirikiano wa kijamii kupitia shughuli mbalimbali za kibiashara.

“Ninamshukuru na kumpongeza sana Mkurugenzi wa Kisangara Tours Ltd Frida Mberesero, kwa kazi kubwa ambayo umeifanya ya kuviibua na kuvionesha vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo wilaya hapa, ambavyo tutavitumia kama sehemu ya kuchochea utalii ndani ya wilaya yetu,”alisema DC Mnkunda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kisangara Tours Ltd, Frida Mberesero, aliwataka wananchi kufanya utalii wa ndani ili kukuza kipato na Uchumi wa nchi huku  akiwaomba viongozi wa Serikali za Vijiji na Kata yaliko maeneo yenye vivutio hivyo, yakiwemo maporomoko ya maji, kuhakikisha yanalindwa na kutunzwa.


Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Kiseo Nzowa, akimkabidhi Tunzo ya shukrani  Mkurugenzi wa Kisangara Tours Ltd, Frida Mberesero, kwa kutangaza vizuri  vivutio vya utalii  vilivyomo Wilayani Mwanga.
Mkurugenzi wa Kisangara Tours Ltd, Frida Mberesero akipongezwa kwa kufanya vizuri kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo Wilaya ya Mwanga.
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bi. Mwanahamisi Munkunda
Mkurugenzi wa Kisangara Tours Ltd, Frida Mberesero, akionesha Tunzo aliyokabidhiwa baada ya kuibuka mshindi wa kuvitangaza vivutio vya utalii vilivomo Wilaya ya Mwanga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.