MOSHI-KILIMANJARO
Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi, kutoka hospitali ya rufaa ya
Bombo-Tanga, Maunt Meru Jijini Arusha, Manyara, hospitali ya rufaa ya mkoa
Mawenzi, KCMC, Benjamini Mkapa na hospitali ya rufani ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi
ya Kibong'oto (KIDH),wameanza kutoa huduma katika hospitali ya rufaa ya Mkoa Mawenzi
ili kuwapunguzia ghalama kwa kufuata huduma hizo katika hospital kubwa nchini.
Hayo yamesemwa na Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa mkoa Mawenzi Dk.
Edna-Joy-Munisi, wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi wa Dk. Samia Kanda ya Kaskazini, na kusema kuwa tangu zoezi hilo lianze
kufanyika Desemba 2 mwaka huu, wamefanikiwa kuona jumla ya wagonjwa 1,328 kati
yao wagonjwa 22 tayari wamefanyiwa upasuaji.
“Ninawashukuru madaktari bingwa na bingwa bobezi waliopo hospitalini
hapana waliotoka mikoa jirani kwa kukubali kuja kutoa huduma hizi hapa
Kilimanjaro, najua ni jukumu zito lakini wamejitoa kuja kutuhudumia,”amesema
Dk. Munisi.
Dk. Munisi amesema, wateja wengi wameendelea kujitokeza katika hospitali
hiyo,huku wengi wao wakiwa ni wanawake
ambao wamekuwa wakifika kwa dakatari bingwa wa wanawake na uzazi,
daktari wa magonjwa ya ndani, sanjari na daktari bingwa wa upasuaji.
Akizindua kambi ya madaktari bingwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin
Babu, amesema serikali ya awamu ya sita imefanya mapinduzi makubwa katika sekta
ya afya hapa nchini.
“Leo tunajionea mapinduzi makubwa katika hospitali zetu za rufaa za
mikoa kwa kuwa na miundombinu, vifaa na vifaa tiba, na hivyo kuwezesha huduma
za kibingwa na bingwa bobezi kutolea kama ambavyo leo hii katika hospitali yetu
ya rufaa ya mkoa Mawenzi,”amesema.
Amesema maboresho hayo yanakwenda sanjari na kutoa ajira katika sekta ya
afya, ambapo katika hospitali ya mkoa Mawenzi
imepokea waajiriwa wapya 64 wa kada mbalimbali.
Babu, amesema katika kuhakikisha huduma za afya zinaimarika kwa wananchi
wake, serikali imekuwa na utaratibu wa kufanya huduma za Mkoba, kibingwa na
bingwa bobezi, katika mikoa mbalimbali hapa nchini, ikilenga wananchi wapate huduma
za afya ndani ya mikoa yao na kwa mkoa wa Kilimanjaro jumla ya huduma 19
zitatolewa na timu ya wataalam hao wa afya.
“Wale wote waliofika hapa kwa ajili ya changamoto mbalimbali za kiafya, watapata
ufumbuzi na Mungu akipenda wataondoka hapa wakiwa wamepona kabisa na kuendelea
na shughuli zao za kiuchumi,”amesema.
Amesema kuwepo kwa kwa madaktari hao bingwa na bingwa bobezi, ni moja ya
fursa kwa wananchi kuweza kufikiwa na kupata huduma za afya bora na za
kitaalamu.
Naye Mganga Mfawidhi hospitali ya Rufaa mkoa wa Tanga Dk. Frank Shega,
amesema katika kuhakikisha huduma za afya kwa wananchi zinaimarika, uboreshaji
wa miundombinu, vifaa tiba, mashine za vipimo,
“Utaratibu wa kuwalipia madaktari bingwa kwa ajili ya kwenda kusomea
ubobezi, umesaidia kuweza kurudi kwa jamii kwa ajili ya kuweza kuwasaidia kutoa
huduma za afya kwa wananchi, badala ya wananchi kwenda katika hospitali za
rufaa za Kanda au hospitali za rufa za Kitaifa.”amesema Dk. Shenga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushsuri ya hospitali ya rufaa ya mkoa Mawenzi, Boniphace
Clement Panga, amesema huduma za kibingwa wananchi walikuwa wakizifuata katika
hospitali za rufaa, kutokana na serikali kuwa sikivu imeamua
kuzisogeza karibu kule wanakotoka.








