Dkt. Hassan Abbasi, amekabidhi gari kwa Mkuu wa Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) Moshi

Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali Watu  Bi. Shani Kamala (kulia) akimkabidhi gari aina ya Land Cruzer Prado TXL Mkuu wa Chuo cha Viwanda vya Misitu FITI Moshi  Dkt. Zacharia Lupala.

MOSHI-KILIMANJARO.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi, amekabidhi gari kwa Mkuu wa Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) ikiwa nia hadi yake aliyoitoa Novemba 1,2024 alipokuwa mgeni rasimi katika mahafi ya 27 ya chuo hicho.

Akikabidhi gari hiyo kwa niaba ya Katibu Mkuu, Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali Watu Shani Kamala, amekabidhi gari hilo Novemba 5, 2024 kwa mkuu huyo wa Chuo Dkt. Zacharia Lupala.

Kamala amesema Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi, alimuahidi Mkuu wa Chuo cha Viwanda vya Misitu FITI Moshi, kumpatia gari aina ya Land Cruzer Prado TXL yenye namba ya usajili STL 6702 na mimi ameniagiza kwa niaba yake kuja kulikabidhi gari hili.” amesema.

Aidha Kamala amesema kutolewa kwa gari hilo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha  utendaji kazi wa taasisi hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Zacharia Lupala, amemshukuru Katibu Mkuu kwa kutoa gari hilo, akieleza kwamba litamsaidia kuongeza ufanisi wa kazi katika majukumu yake.

“Nimetoka kupokea gari ambalo Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, alielekeza linunuliwe kwa ajili ya ofisi ya mkuu wa chuo katika kuimarisha utendaji kazi wangu na gari hiyo nimekabidhiwa leo,”amesema DKt. Lupala.

Amesema gari hiyo ataitumia kwenye shughuli za utawala kaka ilivyokusudio lake katika kuboresha ufanisi na utendaji kazi wa taasisi yake.

“Ninaishukuru sana Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa namna inavyotuongoza na kutuelekeza na kutusaidia katika kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabi na kuweza kutekeleza majukumu yetu, ambayo tumekuwa tukiyafanya kila siku katika kutoa mafunzo ya viwanda vya misitu Moshi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.