MOSHI-KILIMANJARO
Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji mkoani Kilimanjaro, limepiga marufuku wananchi ambao wamekuwa wakinunua
vimiminika na kuhifadhi kwenye vidumu, kopo na kwenye chupa za plasiti, kisha
kuhifadhi majumbani mwao, kuacha mara moja ili kupunguza majanga yanayotokana
na moto.
Kauli hiyo imetolewa na
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu
Jeremiah Mkomagi, wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye kilele cha
oparesheni ya mafunzo ya pamoja kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka
Jiji la Marburg Nchini Ujerumani.
Mkomangi amesema ni
hatari kuwa na vimiminika vya moto ndani ya nyumba na kuwataka wananchi
kuchukua tahadhari ili kuweza kuzuia majanga kama hayo yasiweze kutokea.
Aidha alisema Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji mkoani humo, limefanya oparesheni ya pamoja kati ya Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji kutoka Jiji la Marburg nchini Ujerumani.
Amesema ushirikiano
huo umekuja baada ya kuingia makubaliano ya kimiji baina ya Manispaa ya Moshi
na Ujeruni kwa kipindi cha miaka miwili.
Nao baadhi ya
wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Lucy Lameck, iliyoko Manispaa ya Moshi ambao
wako katika Klabu ya kujitolea ya Jeshi la Zimamoto na Ukoaji Manispaa ya
Moshi, walielezea namna walivyofundishwa kuhusu matumizi ya vifaa na mbinu
mbalimbali za matumizi ya vifaa hivyo kama ambavyo wanaeleza.
Akizungumza Mganga mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Jairy Khanga amesema ushirikiano huo baina ya
Manispaa ya Moshi na Jiji la Marburg nchini Ujerumani, utaleta faida chanya,
ikiwemo hospitali ya rufaa ya mkoa Mawenzi.









