
Mwenyekiti wa Jimbo la Moshi Vijijini (Chadenma) Jumanne Mwenga , akikabidhi kadi ya Chadema kwa Mlezi wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Rabia Abdallah Hamid.
MOSHI-KILIMANJARO
Mlezi wa CCM MKoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Rabia Abdallah Hamid, amewapokea wanachama 10 kutoka Chama cha DEmokrasia na Maendeleo (chadema) ambao wameamua kurudi CCM.
Wanachama hao wamepokelewa leo Oktoba 16, 2924 wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jimbo la Moshi Vijijini wa chama hicho Jumanne Mwenga, ambae amekihama chama hicho na kujiunga na (CCM) na kusema kuwa ameridhika na kazi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuamua kumuunga mkono.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Mwenga amesema “Nilikuwa Mwenyekiti
wa Jimbo la Moshi Vijijini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nimehudumu
kwenye chama hicho kwa kwa kipindi cha
miaka minane, ndugu zangu nimefika mahali nikaona kama ninaendelea ‘kuchoka’…..
nimefanya kazi ya kukijenga chama, lakini nikafika mahali nikaona kwa nini ninaendelea
kuumia, nikaamua kusepa zangu.”amesema Mwenga.
Aidha maesema kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu ya uongozi wa rais Samia Sulu Hassan, yako mambo mengi ya maendeleo yamnefanyika ambayo ndio tulikuwa tunayahitaji kama wananchi.
Amesema ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kafanya mambo mengi yaliyo
tukuka, nikaona sasa mimi ni nani niendelee kubaki Misri, nikaona ni vema
niungane na timu ya watu wa maendeleo ambayo ni CCM.
Ameongeza kusema “Kama wananchi tumeyapata tuliyokuwa tunayataka nitafute nini tena huko Chadema?..ninaushukuru sana uongozi wa CCM mkoa kwa kazi kubwa ya kuhamasisha maendeleo na kuzitawanya fedha ambazo zilikuwa zinaletwa na serikali kuu ambazo zimekuja kwenye Kata yangu ya Mabogini kuwezesha kujenga hospitali mpya ya wilaya, lakini pia tumepata na zahanati kwenye vijiji.”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Patrick
Boisafi amesema kurudi kwa wanachama hao ndio tafsiri halisi ya R4 za
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia
Suluhu Hassan.
Akiwapokea mbele ya Hadhira ya wanachama mkoani humo Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Rabia Abdallah Hamid amesema Serikali
inayoongozwa na Rais Samia imeleta fedha nyingi za maendeleo ndio maana wanachama
walioko upinzani wanaamua kuunga na chama chenye ushindi.
Hata hivyo Rabia amewaasa wanachama wa CCM mkoa wa
Kilimanjaro kuwa Uongozi ni alama hivyo wanapaswa kuutendea haki inavyostahili.
Katika hatua nyingine Rabia amemtaja Mchungaji Peter Msigwa ambaye awali alikuwa Mbunge Iringa Mjini na kada wa Chadema kuwa CCM inaendelea kufanya vema kwa ajili ya Maendeleo ya Watanzania.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Rabia amekuja mkoani Kilimanjaro wakati ambao
zoezi la Uandikishaji wa orodha ya Wapiga Kura likiendelea ambalo linatarajiwa
kumalizika mnamo Oktoba 20, 2024; kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali Mitaa
utakaofanyika Novemba 27, mwaka huu.






