Serikali mkoani Kilimanjaro, imesema kuwa uhakifu mwingi unaotokea katika jamii kwa sasa unasababishwa na matumizi mabaya ya akili inayopelekea baadhi ya vijana kufanya uhalifu uliopitiliza.
Hayo yamo kwenye taarifa ya Mkuu wa mkoa huo Nurdin Babu, iliyosomwa kwake na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Zephania Sumaye, wakati wa ufunguzi wa kongamano la vijana mkoani humo, lililoandaliwa na Taasisi ya Tanzania Ex-Prisoners Foundation (TEPF) likiwa na lengo mahususi kwa ajili ya kuwakumbusha vijana juu ya kutokujiingiza katika vitendo vya kihalifu.
Amesema kutokutumia akili ya kuweza kujipatia kipato panapokuwa na uhitaji au tamaa iliyopitiliza inapelekea vijana walio wengi kuweza kujiingiza kwenye vitendo vya kihalifu.
Sumaye amesema kuwepo kwa kongamano kama hilo, litasaidia vijana ambao hawajaanza kujiingiza kwenye uhalifu kufundishwa kwa nini uhalifu unatokea katika jamii.
Mkuu huyo wa Wilaya amewataka vijana kufanya kazi kwa bidii kwa kutumia akili zao vizuri illi kuweza kutengeneza kipato chao, wakiweza kuwa na kipato imara hata vitendo vya kihalifu vinaweza kupungua kwenye jamii.
Aidha alitwka jukwaa hilo, litumike kuwa fursa ya kujitafakari wapi wamekosea ili kuweza kujirekebisha jambo ambalo litakwenda kujenga jamii iliyo bora na isiyo na matukio ya kihalifu
"Yako matukio mbalimbali ya uhalifu ambapo vijana wamekuwa pia wakitajwa kujihusisha na matukio ya kihalifu ambapo vijana, watoto na wanawake wakiwa wahanga wa matukio hayo ya uhalifu yanayoripotiwa katika jamii."amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi isiyo kuwa ya Kiserikali ya Tanzania Ex-Prisoners Rose Malle, amesema lengo la kongamano hilo ni kuwaelimisha vijana kuzitambua sababu zinazopelekea kujiingiza kwenye uhalifu na kuwapa elimu ya namna ya kuepukana na vishawishi vitakavyo wasababisha wao kujiingiza katika makundi hayo mabaya.
"Takwimu zinaonesha kwamba asilimia kubwa ya wafungwa wanaomaliza vifungo vyao gerezani wanaporudi uraiani, wamekuwa wakirudia tena uhalifu na kurejeshwa gerezani na kwamba taasisi hiyo imekuwa ikiandaa matamasha na makongamano kama hays ili kuwapatia elimu kwa wale wafungwa ambao wamekwisha kutoka gerezani,"amesema Malle.
Akizungumza na KISENA BLOG iliyotaka kufahamu ni kwa namna gani viongozi wa dini katika kuwafanya vijana waepuke mitego ya uhalifu pamoja na utumiaji wa dawa za kulevya na hapa anafafanua Nabii Esther Bukuku.