Dkt. Shoo ameyasema hayo Agosti 9,2024 wakati wa Ibada ya mazishi ya Mchungaji Kantante aliefariki kwa ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Kimashuku, wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro Agosti 4, mwaka huu.
Katika mahubiri yake Askofu Shoo amewataka waamini kuondokana na dhana isiyo sahihi kwamba kwa kuwa wao ni Wakristo, Watumishi wa mtumishi wa Mungu wako ndani ya Kristo hawawezi kukumbana na dhoruba au changamoto za maisha na kuwataka kuepuka dhana hiyo na badala yake wajiweke tayari bila kujali nyadhifa au nafasi zao walizonazo ndani ya jamii.
Aidha Askofu Shoo amesema marehemu Kantante Munisi enzi za uhai wake, alikuwa mtumishi aliegusa maisha ya watu wengi, alikuwa mtumishi mwema, alikuwa na uhusiano mzuri aliouweka kwa watu wote, alikuwa ni mtuy mwenye kujitoa ambapo pia alikuwa mama na mke aliyetunza familia yake.
Akisoma risala ya marehyemu Naibu Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Munguatosha Makyao amesema, marehemu Mchg. Kantante Fatael Munisi, alizaliwa Mei 9 mwaka 1982, katika Kijiji cha Mpwapwa Jijini Dodoma , akiwa ni motto wa pili wa mzee Fatael Munisi.
Marehemu Kantante Fatael Munisi ameacha mume na watoto wane wa kiume wawili na wakike wawili.
Katika mazishi hayo viongozi mbalimbali walishiriki maziko hayo akiwemo Mbunge wa Jimbo la Hai Saasisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo, Mbunge mstaafu Lucy Owenya.