Dkt. Damas Ndumbaro aagiza Swahili Marathon kutanua wigo


SWAHILI MARATHON, ARUSHA

Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro, amewaagiza wandaaji wa mashindano ya Mbio ndefu za Swahili Marathon, kupanua wigi wa mbio hizo na kufanya kuwa za Kimataifa zaidi.

Dkt. Ndumbaro ametoa agizo hilo Juni 29,2024 wakati akihitimishia msimu wa Piili wa Mbio hizo, zilizofanyika Jijini Arusha, mkoani Arusha.

Amesema kuwa pamoja na kwamba mbio hizo ziko kwenye msimu wa pili, tayari hamasa miongoni mwa washiriki imeonekana kuwa mkubwa ikiwemo washiriki kutoka nje ya nchi jambo ambalo amesema litasaidia kuitangaza Tanzania na lugha ya Kiswahili kwa ujumla.

Aidha Waziri Ndumbaro amewoa maagizo kwa kuwaagiza Waratibu wa Mbio za Swahili Marathon kuhakikisha kuanzia msimu ujao, kuwe na mashindano mawili kwa jina hilo hilo la Swahili Marathon ambapo tukio moja lifanyikie Tanzania na la pili lifanyikie nchini Uganda kwa lengo la kukitangaza Kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania.

Amesema sababu ya kutoa agizo hilo ni ili lugha hiyo ipelekwe nje ya mipaka ya Tanzania ambao ndiyo Waasisi wa lugha ya Kiswahili,  na pia kutokana na ukweli kuwa Uganda ndiyo inayotoa washiriki wengi kuliko mataifa mengine yanayoshiriki mbio hizo.

Vilevile Wzairi huyo ametoa maagizo kwa Uongozi wa Chama cha Riadha nchini (RT) kuendelea na mipango madhubuti inayolenga kuibua vipaji vipya ili Tanzania iwe na washiriki wengi kwenye mashindano ya riadha ya Kimataifa ikiwemo ile ya Olympic. 

Aidha ameesema Wizara hiyo  imeandaa mikakati itakayowezesha uanzishwaji wa timu za Taifa zitakazotokana na wachezaji watakaoibuliwa kutoka kwenye michezo ya Umisseta na Umitashumta. 

Akiongea kwenye hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) Consolata Mushi, amesema zaidi ya watu 300 wameshiriki mbio za msimu wa pili  za Swahili Marathon, mwaka huu.

Kuhusu swala la kuyafanya mashindano hayo kuwa ya Kimataifa, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili Taifa amesema kama sehemu ya waandaaji tumepokea maelekezo ya Waziri na wataanza kulifanyia kazi kwa lengo la kupanua wigo wa michezo hiyo sambamba na lengo lake la kukuza vipaji na lugha ya Kiswahili kwa ujumla.

Nao baadhi ya washiriki wa mashindano hayo, Damian ChristianKasimu Shaban na Koleman Thompsonwametoa Wito kwa waandaaji wa mbio hizo kuzitangaza mapema pamoja na kufanya uzinduzi wake mapema ili watu wengi waweze kujiandaa mapema kutokana na ukweli kuwa watu wengi wanapenda kushiriki michezo ikiwemo za riadha za mbio ndefu.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.