Wakazi wa Kimbale wampongeza Mbunge Tadayo, kutatua changamoto ya maji, barabara

Mbunge wa Mwanga Joseph Tadayo akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kimbale huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuwatumikia wananchi hao ambao wamempongeza kwa kutatua changamoto ya maji na barabara iliyokuwa ikiwakabili. (Picha na KISENA)

KIMBALE, CHOMVU; MWANGA

Wakazi wa kijiji cha Kimbale, Kata ya Chomvu Wilaya ya Mwanga, wamemshukuru Mbunge wa Jimbo hilo Joseph Tadayo, kufanikiwa kuwatatulia changamoto ya maji na barabara iliyokuwa imedumu toka Tanzania kupata Uhuru.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Kijiji hicho, baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa walikuwa wanachangamoto kubwa ya kukosa maji Safi na Salama katika Kijiji hicho na kupeleka kuamka usiku kwenda kutafuta maji umbali mrefu na kufifisha shughuli za kimaendeleo.

Mkazi wa kijiji hicho Shwahibu Mziray, alimpongeza mbunge wa Jimbo la Mwanga kwa jitihada zake kubwa za kutatua changamoto za wananchi waliompa kura.

"Eneo letu la kijiji cha Kimbale lilikuwa na changamoto kubwa ya barabara ambayo ilikuwa haipitiki kabisa, mimi kwa sasa niana miaka (67) nikiwa darasa la tatu ndipo niliona catapira likitengeneza barabara hii, tangu hapo sijawahikuona hadi kipindi chako mbunge,"amesema.

Naye George Mtengeti amesema "Changamoto yetu kubwa iliyokuwa inawakabilia wananchi ni suala la upatikanaji wa maji safi na salama, kabla ya kutatua changamoto ya barabara hii, kulikuwa hakuna gari lolote lililokuwa linafaika kijiji kwetu kutokana na ubovu wa barabara.".

Mkazi mwingine wa kijiji hicho Anjelina Simoni, amemshukuru mbunge wa Jimbo la Mwanga kwa jitihada zake za kutatua changamoto za maji katika kata hiyo.

"Tulikuwa tunakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosa maji Safi na Salama katika kijiji chetu na kupeleka kuamka usiku kwenda kutafuta maji umbali mrefu na kufifisha shughuli za kimaendeleo."amesema Simon.

Akihutubia mamia ya Wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo, Mbunge wa Jimbo la Mwanga Joseph Tadayo, amesema kuwa anafanya kazi ili kuhakikisha wananchi wapata maendeleo kwa wakati ili kuijenga Mwanga mpya na ya kisasa.

"Jitihada za kuleta maendeleo katika tarafa ya Usangi, kata ya Chomvu, kijiji cha Kimbale na vijiji vingine, kubwa kabisa zinatokana na serikali ya CCM inayooongwza na Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa msikivu na sisi Wabunge tunapopeleka vilio vyetu Bungeni, amekuwa tunasikilizwa na kuvitekeleza,"amesema Mbunge Tadayo.

Pia amewataka wananchi kuwapuuza wanasiasa wote wanaoeneza habari mbaya na za uongo kuhusu mbunge huyo kuwa viatu vya kuliletea maendeleo Jimbo hilo havimtoshi;

"Naomba niwaahidi wananchi wa kijiji cha Kimbale na kata ya Chomvu kwa ujumla wake, nitaendelea kuwatatulia changamoto zenu zilizobaki ili ikifika kipindi cha uchaguzi kusiwepo na maswali ya kuniuliza kutokana na kazi kubwa za kimaendeleo ninazozifanya jimboni.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.