Taasisi ya Ndesamburo mbioni kukusanya uniti 300 za damu

Mkurugenzi wa PNF Lucy Owenya (wa tatu kutoka kushoto) akikabidhi msaada wa hali na mali kwa wahanga wa mafuriko wa Kijiji cha Korini Juu, Kata ya Mbokomu. (Picha na KISENA)


TAASISI ya Philemon Ndesamburo Foundation (PNF) iliyoko Moshi, mkoani Kilimanjaro, inatarajia kuandaa kambi ya uchangiaji damu, ambapo inatarajia kukusanya jumla ya unit 300 za damu kupitia kambi hiyo.

Hayo yameelezwa jana na Meneja wa Redio ya Moshi FM Lewis Ringo, wakati wa hafla ya kukabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu kwa familia zilizokumbwa na maafa ya mafuriko ya mvua kubwa yaliyotokea katika maeneo mbalimbali ndani ya kijiji cha Korini-Juu Kata ya Mbokomu Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, mwishoni mwa mwezi wa nne.

“Kambi hii inayotarajiwa kufanyika Mei 26 mwaka huu, ikiwa ni mwendelezo wa matamasha ya kila mwaka ya kumbukumbu ya aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro Hayati Philemon Ndesamburo”, alisema.

Alisema Taasisi ya Ndesamburo Foundation kwa kushirikiana na Moshi FM,  tutakuwa na tamasha la uchangiaji damu zoezi litakaloendeshwa na Kituo cha Damu Salam, kooichoko Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC, ambapo pia kutakuwa na upimaji wa afya bure ya magonjwa aina mbalimbali yakiwemo yale yasioambukizwanzoezi ambalo litaendeshwa na wataalamu wa afyakutoka hospitli ya Jaffar iliyoko mjini Moshi.

“Kambi hii itawekwa katika uwanja wa shule ya msingi ya Nelson Mandela iliyoko Kata ya Pasua Manispaa ya Moshi, ambapo pia kutakuweko na burudani mbalimbali kama vile mpira wa miguu kwa maveterani pamoja na tamasha la mziki utakaohusisha pamoja na watumbuizaji wengine, wasanii wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva”, alisema.

Akikabidhi misaada hiyo kwa familia iliyoondokewa na mtoto wa miaka 13 aliyefariki kwa kuangukiwa na ngema na nyumba yao kuezuliwa na tope Mkurugenzi wa Makampuni ya Keys Lucy Owenya; alisema kuwa kampuni hiyo imetoa misaada mbalimbali ya kibinadamu kama mchele, mahindi, maharagwe, sabuni kwa wahanga hao, lengo likiwa ni kuendeleza aliyokuwa akiyafanya mwaasisi wa Taasisi hizo Hayati Philemon Ndesamburo ya kurejesha faraja kwa jamii.

“Wakati wa uhai wake Mzee Ndesamburo alikuwa alijikita zaidi kwa kutoa michango aina mbalimbali ndani ya jamii ambayo sisi wana familia tumeamua kuienzi kila mwaka kwa kuifanya  kuwa sehemu ya kumbukizi ya kile alichoamini na kukiishi”, alisema.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.