DODOMA, TANZANIA
Tanzania, inayojulikana rasmi kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hipo Afrika Mashariki ndani ya ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika. Imepakana na Uganda upande wa kaskazini; Kenya upande wa kaskazini mashariki; Visiwa vya Comoro na Bahari ya Hindi upande wa mashariki; Msumbiji na Malawi upande wa kusini; Zambia kuelekea kusini magharibi; na Rwanda, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi. Pia mlima Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika unapatikana kaskazini mashariki.
Tanzania ya Kale
Mabaki ya viumbe wengi walioishi zamani yamepatikana Tanzania katika historia, mfano ni watu walioishi miaka milioni 6 iliyopita walioitwa “Pliosini” (Pliocene). Pia watu waitwao “Australopithekasi” (Australopithecus) walioishi kati ya miaka milioni 4 hadi milioni 2 iliyopita; na mabaki ya watu wengine wa aina ya Homo yaligundulika pia na kupatikana karibu na Ziwa Olduvai. Kufuatia kuongezeka kwa Homo erektasi (Homo erectus) miaka milioni 1.8 iliyopita, ubinadamu uliweza kuenea kote katika Ulimwengu wa zamani, na baadaye katika Ulimwengu Mpya na Australia kama jamii iliyojulikana kama Homo Sapiensi (Homo sapiens).
Homo sapiensi pia walijaza Afrika nzima kufanya jamii zingine za binadamu kupunguwa au kupotea kabisa. Moja ya makabila ya zamani zaidi yanayojulikana bado yapo, Hadzabe, yanaonekana kuwa na asili ya Tanzania, na historia yao ya mdomo inaonyesha kwamba wazee wao wa kale walikuwa warefu na wa kwanza kutumia moto, dawa, na waliishi katika mapango, kama Homo esingasi (Homo eisengus) au Homo Heidelibergensisi (Homo heidelbergensis) ambao waliishi katika eneo hili hili la Tanzania kabla yao.
Tanzania ya Sasa
Umoja wa Mataifa ulikadiria idadi ya watu wa Tanzania 2018 kuwa milioni 56.31, ambayo ni chini kidogo kuliko Afrika Kusini. Idadi hii umeifanya Tanzania kuwa nchi ya pili yenye watu wengi kabisa kusini mwa Ikweta. Idadi ya watu inajumuishwa na makabila karibu 120, lugha, na dini mbalimbali. Mji wake mkuu rasmi ni Dodoma ambapo ofisi ya raisi, Bunge la taifa, na wizara kadhaa za serikali ziko. Dar es salaam, mji mkuu wa zamani, una ofisi nyingi za serikali na ndio mji mkubwa zaidi nchini, bandari kuu, na kituo kikuu cha biashara.