MOSHI.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava, ametoa onyo kali kwa watu wote wanaohusika na ukataji miti na uchomaji mkaa ndani ya hifadhi ya msitu wa asili wa Kahe, akiwataka kujisalimisha ndani ya siku saba au wakumbane na mkono wa sheria bila msamaha.
Kauli hiyo ameitoa jana katika zoezi la uoteshaji miti lililofanyika katika msitu huo, Mnzava ameeleza kuwa tayari watu saba wamebainika kuhusika na uharibifu huo wa mazingira na kwamba vyombo vya usalama kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) vinaendelea kuwatafuta.
Kwa upande wake Mhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Moshi, Godson Ullomi,amesema changamoto ya uvamizi wa misitu ndani ya hifadhi ya msitu ya asili ya Kahe inaendelea kutishia uhai wa mazingira katika wialaya hiyo.
Amesema baadhi ya wananchi wanachoma mkaa, hukata miti ovyo kwa kuni, kuingiza mifugo hifadhini na hata kuchoma moto misitu kiholela.
Kauli hiyo ameitoa jana katika zoezi la uoteshaji miti lililofanyika katika msitu huo, Mnzava ameeleza kuwa tayari watu saba wamebainika kuhusika na uharibifu huo wa mazingira na kwamba vyombo vya usalama kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) vinaendelea kuwatafuta.
Amewataka wale wote ambao wanaendelea kutafutwa wamekimbia na kutoroka, amewapa kipindi cha siku saba wajisalimishe kwa TFS au ofisi yoyote ya serikali na huo ndio msamaha pekee kwani baada ya hapo msako utaendelea bila msamaha.
Mkuu huyo wa wilaya akaweka wazi kuwa hakuna mtu atakayeruhusiwa kukata mti, hata kama upo kwenye shamba lake mwenyewe, bila idhini ya maandishi kutoka kwake huku akisistizam kuwa vibali vyote vya uvunaji miti ni lazima vipitie kwake, na yeyote anayetoa vibali kinyume na utaratibu “safari yake imefika mwisho.”
Amewataka wenyeviti wa vijiji, watendaji wa vijiji na kata, pamoja na maafisa tarafa kuhakikisha wanachukua hatua haraka kwa yeyote atakayebainika kukata miti bila kibali halali.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya amewatahadharisha wafugaji wanaoingiza mifugo kwenye maeneo ya hifadhi na taasisi za elimu, akisema kuwa mifugo hiyo itaweza kutaifishwa ikiwa itaonekana katika maeneo hayo.
Naye Diwani wa Kata ya Kahe Magharibi, Aloyce Mumbuli, amesema kata hiyo ina misitu miwili ya asili (Kahe namna moja na Kahe namna Mbili), amesema wako baadhi ya watu wameendelea kuharibu misitu hiyo kwa kukata miti kwa lengo la kuchoma mkaa, licha ya juhudi za utoaji elimu wa mara kwa mara.
Amesema baadhi ya wananchi wanachoma mkaa, hukata miti ovyo kwa kuni, kuingiza mifugo hifadhini na hata kuchoma moto misitu kiholela.