MOSHI.
Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Priscus Tarimo, amewashukuru wananchi wa Moshi na Rais Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio makubwa ya miradi ya maendeleo katika jimbo lake.Aidha alitoa wito kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa na wan-CCM kwa ujumla kuacha tabia ya kusalitiana, ambapo alisema imekuwa chanzo kikuu cha kuyumbisha baadhi ya vyama vya upinzani nchini.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Soko la Manyema, mjini Moshi, Tarimo alisema tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 Jimbo la Moshi Mjini lilikuwa likiongozwa na vyma vya upinzani na anguko la CCM halikusababishwa na vyama vya upinzani bali ilisababishwa na Wan-CCM wenyewe kwa kuzungukana na kwenda kukipigia kura chama cha upinzani.
“Mhe; mgeni rasmi CCM hatujawahi kuanguka kwa sababu ya upinzani, tunaanguka kwa sababu ya kuzungukana, hizi dua zilizopigwa hapa na viongozi wa dini zikafukuze roho ya kuzungukana!” alisema Tarimo kwa hisia kali.
Mbunge huyo pia alitoa salamu maalum za shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kauli yake ya wazi aliyoitoa hivi karibuni wakati akifunga Mkutano Mkuu wa CCM, akieleza kuwa hajatuma mtu yeyote kugombea nafasi ya uongozi, hivyo akawataka wote wanaojihusisha na siasa kujitokeza wazi kupambana kwa hoja na si kwa mgongo wa urafiki wa kisiasa.
“Tunaomba utupelekee salamu za shukrani kwa Rais Samia kwa kazi hizo zote, lakini mimi binafsi naomba umpelekee shukrani kwa kauli yake wakati anafunga mkutano mkuu juzi, hasa pale aliposema hajatuma mtu. Maana kuna watu walishatuonyesha hadi namba, wakisema wametumwa, Sasa kwa sababu hajatuma mtu, uwanja uko wazi, twendeni tukapambane,” alisema Tarimo.
Tarimo alitaja utekelezaji wa ahadi 9 kati ya 10 alizoziahidi mwaka 2020 wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, huku akisema kwa asilimia 90 ya miradi hiyo imetekelezwa hivyo Rais Samia anastahili kupewa kura kwa kazi alizozifanya.
Mbunge huyo alitaja baadhi ya miradi iliyokwisha kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Moshi, ambayo iko katika Kata ya Ng'ambo, ikiwa ni ya ghorofa na kugharimu zaidi ya Sh bilioni 6.5.
Alisema katika vituo vya afya Tarimo alisema Serikali imejenga vituo vya afya viwili ambapo kimoja kimejengwa Kata ya Shirimatunda na kingine Msandaka, na cha tatu (kiboriloni) ambacho kitapandishwa hadhi kuwa kituo cha afya kufikia Juni 30, kwa kutumia Sh milioni 250.
Mbunge huyo alitaja baadhi ya miradi iliyokwisha kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Moshi, ambayo iko katika Kata ya Ng'ambo, ikiwa ni ya ghorofa na kugharimu zaidi ya Sh bilioni 6.5.
Alisema katika vituo vya afya Tarimo alisema Serikali imejenga vituo vya afya viwili ambapo kimoja kimejengwa Kata ya Shirimatunda na kingine Msandaka, na cha tatu (kiboriloni) ambacho kitapandishwa hadhi kuwa kituo cha afya kufikia Juni 30, kwa kutumia Sh milioni 250.
Katika sekta ya elimu; alisema Ujenzi wa madarasa zaidi ya 400, shule mpya tatu za sekondari ya Msandaka, Lucy Lameck, na Kaloleni, zote zimeanza kutoa huduma huku shule ya mchepuko wa Kiingereza imeanzishwa kupitia mapato ya ndani na kupewa jina la JK Nyerere.
Aidha alisema miradi mingine imejengwa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) ambako kuna ujenzi wa jengo jipya la ICT Sh bilioni 3.5 jengo la mihadhara Sh bilioni 6.8 na maktaba inayogharimu Sh bilioni 8.9.
Kuhusu sekta ya michezo:, alisema uwanja mpya wa mpira wa miguu unajengwa katika Kata ya Majengo kupitia mapato ya ndani, huku Serikali ikitoa Sh bilioni 12 kwa ajili ya ujenzi uwanja wa ndege wa Moshi:
Alisema soko la Mbuyuni lililoungua kwa moto mara mbili, lakini serikali imeleta gari la zimamoto kusaidia huduma za dharura.
Mbunge Tarimo alihitimisha kwa kuwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia, akisisitiza kuwa kazi imefanyika na sasa ni muda wa kuhakikisha miradi hiyo inalindwa na kuendelezwa kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi zote.












