Mafisa usafirishaji watakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarania

MOSHI-KILIMANJARO

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi Mjini Faraji Swai, amewataka maafisa usafirishaji (Bodaboda na Bajaj) na watumiaji wengine wa vyombo vya moto barabarani mkoani Kilimanjaro kutii sheria bila shuruti ili kupunguza ajiali zisizo na ulazima.

Wito huo umetolewa Septemba 3,2024 wakati wa halfla fupi ya kukabidhi Cheti cha Wakala wa kutoa Leseni za LATRA kwa Chama cha Ushirika na Mikopo cha Bajaji na Bodaboda mkoani Kilimanjaro (KIBABOT SACCOS) kilichofanyika Ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.

Sawi amewataka madereva hao, kuendelea kuwa mabalozi wazuri  wa kutii bila shuruti sheria za usalama barabarani kwa kuhakikisha wanakuwa salama wao na abiria  waliowapakiza katika vyombo hivyo vya moto.

“Niwapongeze kwa hatua hii nzuri ya kuanzisha SACCOS, ambapo leo mnakwenda kukabidhiwa cheti cha Wakala wa kutoa Leseni za LATRA, niwaombe wale wote ambao wameingia katika sekta ya usafirishaji kwa kutumia bodaboda na bajaj nendeni pia mkawaelimisha na vijana wengine kutii sheria za usalama barabarani.”amesema Faraji Swai.

Pia amesema Serikali inatambua kuwa Vijana ni nguvu kazi na rasilimali ya maendeleo ya Taifa lolote lile ulimwenguni hivyo Serikali imeona umuhimu wa kuweka Sera na Mipango madhubuti kwa Vijana sambamba na kuanzisha Idara, Mabaraza na Jumuiya za Vijana kwa lengo la kuhakikisha maendeleo ya Vijana yanapatikana.

“Sera mpya ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2023 imedhamiria kuimarisha na kuwekeza zaidi katika kukuza ustawi na maendeleo ya vijana nchini hasa katika Sekta ya Elimu, Afya, Utawala bora, Uwekezaji, Ajira, Ubunifu, Teknolojia ya Habari ba Mawasiliano (TEHAMA).”

Aidha Mwenyekiti huyo wa CCM Wilaya ya Moshi Mjini amezishukuru taasisi mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA na Ofisi ya Usalama Barabarani Mkoa wa Kilimanjaro kwa kuweza kuwaunganisha vijana hao na hatimaye kuanzisha SACCOS yao.








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.