Naibu Katibu Mkuu wa (CCM) Bara Agrey Mwanri akivishwa Skafu baada ya kuwasili ofisi za CCM mkoa wa Kilimanjaro Septemba 22,2026.
MOSHI-KILIMANJARO.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Aggrey Mwanri, anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku saba mkoani Kilimanjaro, ikiwa na lengo la kukagua uhai wa chama, kusalimiana na wananchi, kusikiliza kero zao na kushiriki katika jitihada za kuzitafutia ufumbuzi.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Abraham Urio, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara hiyo.
Urio amesema ziara hiyo itahusisha mikutano ya ndani ya chama pamoja na mikutano ya hadhara, ambapo Naibu Katibu Mkuu huyo atapata fursa ya kuzungumza na wananchi katika maeneo mbalimbali ya mkoa.
Urio amesema ziara hiyo itahusisha mikutano ya ndani ya chama pamoja na mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali ya mkoa, ambapo Mwanri atapata fursa ya kuzungumza na wananchi na kusikiliza changamoto zinazowakabili.
Amesema Septemba 22, mwaka huu, Mwanri ataanza ziara hiyo katika Manispaa ya Moshi kwa kufanya kikai cha ndani, baadaye mchana mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Manyema, kabla ya Septemba 23 kuelekea Wilaya ya Siha, ambako atafanya mkutano katika Viwanja vya CCM.
Kwa mujibu wa Urio, Septemba 24, Mwanri atakuwa Wilaya ya Same Magharibi, ambako atafanya mkutano wa hadhara katika Shule ya Msingi Makanya, na baadaye ataelekea Same Mashariki kwa ajili ya mkutano mwingine utakaofanyika katika Viwanja vya Ndungu.
Amesema Septemba 25 na 26 Mwanri atakuwa na mapumziko, kabla ya kuendelea na ziara hiyo Septemba 27 katika Wilaya ya Rombo, ambako atafanya mkutano wa hadhara Tarake.
![]() |
Amesema ziara hiyo itahitimishwa Septemba 30 katika Wilaya ya Hai, ambapo Mwanri atafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Snow View.
Aidha, Urio amesema ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za CCM kuendelea kuimarisha uhai wa chama, kujenga ukaribu na wananchi na kusikiliza maoni pamoja na changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro.![]() |
![]() |
![]() |
![]() |

















